TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TANKI LA MAJI SOMELO
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TANKI LA MAJI SOMELO
WILAYA YA ILALA, MKOA WA DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inatekeleza mradi wa uboreshaji huduma za majisafi katika maeneo ya pembezoni mwa mji ambayo hayajafikiwa na mtandao rasmi wa DAWASA.
Mradi huu unatekelezwa na DAWASA kwa ufadhili wa benki ya dunia katika Wilaya ya Ilala ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika Manispaa ya Ilala, ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji la ujazo wa lita milioni 2, unaendelea katika Kata ya Zingiziwa.
Utekelezaji huu unahusisha ulazaji wa bomba za maji kwa umbali wa kilomita 16.8 ambapo katika hizo, kilomita 1.78 ni bomba kuu la inchi 10 linalotoa maji katika kisima cha Nzasa na kupeleka maji katika tanki la Somelo na kilomita 15 ni mabomba madogo madogo ya usambazaji kwa wananchi yenye ukubwa wa inchi 8, 6, 4, 3, na inchi 2.5.
Aidha mradi huu umehusisha ufungaji wa pampu yenye uwezo wa kusukuma maji lita elfu 60,000 kwa saa kwa umbali wa mita 160, ambapo chanzo chake cha maji ni kisima chenye urefu wa mita 580 kilichopo eneo la Nzasa chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 216,000 kwa saa.
Kwa sasa mradi huu umefikia kwa asilimia 82 ya ukamilishaji wake, na jumla ya wakazi 10,500 katika mitaa ya Nzasa pamoja na Somelo wanatarajiwa kunufaika pindi mradi huu utakapokamilika.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na DAWASA kwa mwaka 2021/2022 ili kuweza kukidhi agizo la Serikali la kuhakikisha ifikapo 2025 upatikanaji wa huduma ya maji unafikia 85% na 95% kwa maeneo ya vijijini na mijini sawia.
2.0 Gharama ya mradi
Mradi huu kwa ujumla utakaogharimu kiasi cha bilioni Tsh. 1,512,277,699 ni Bila VAT. Mradi unatekelezwa na Mkandarasi M/S Advent Co. Ltd. na msimamizi wa mradi huu ni kampuni ya WAPCOS Ltd kwa kushirikiana na Galaxy Project Services Ltd.
